Sunday, July 8, 2012

Ukumbi maarufu Mamba Disco Kenya, kuwa ukumbi wa Injili


Mombasa, Kenya. Wamepata ukumbi mkubwa kwa ajili ya matamasha ya Injili, ukumbi huo maarufu kama MAMBA DISCO ilikuwa ni club ya waimbaji wasio wa kikristo, sasa unafanyiwa matengenezo na itakuwa zinapigwa nyimbo za Injili tu, mmiliki wa ukumbi huo  Hezron Awiti Bolo amesema lengo lake ni kuitangaza Injili kupitia ukumbi wake na kuwainua waimbaji wa nyimbo za Injili wajulikane.

Ukumbi utazinduliwa rasmi March 2013. Inatazamiwa kuzinduliwa na waimbaji na wahubiri wa kimataifa

Itakuwaje kama hapa Tz tukisikia club bilicanas na nyinginezo zimevunjwa kuwa kanisa au imebadilishwa kuwa kumbi za nyimbo za Injili?

Bado swali linakuja Je waimbaji wa Injili haitakiwi kukubali mialiko kwenye kumbi zisizo za Kikristo? Kumbi za Kikristo ni kumbi gani?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...