Thursday, July 19, 2012

Fahamu asili na maana ya jina lako!
Ni vizuri kuelewa jina lako na maana yake, kuna mambo mengi hukutokea kwa uzuri au ubaya lakini yawezekana na jina lako linachangia au asili ya jina lako …Kuna wengi wetu wamepewa majina yao kutoka kwa mababu zao ambao walikua na roho fulani labda ya umasikini, uzinzi, magonjwa n.k. Wengine wamepewa majina kutoka kwa waganga wa kienyeji au mizimu, ndio maana kuna vifungo fulani unavyo kwenye maisha yako. Jina lako linang’ang’ania ubaki pale pale, hakuna kusonga mbele, wewe ni wa hivyo hivyo au unajimilikisha magonjwa  fulani kwasababu bibi au babu zako walikua nayo. Mfano unasema mimi ugonjwa wangu ni kisukari, TB au sie kwetu ndio ugonjwa wetu! nk
Jina lako lilivyo ndivyo ulivyo!
NABALI – 1Samweli 25:25 “Nakusihi, Bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma”.
Baadhi ya watumishi wa Mungu ambao majina yapo yalibadilishwa
YAKOBO – Mwanzo 32:26-28..”Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.  Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
IBRAHIM – Mwanzo 17:4-6.. “Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.”
Bila shaka unawafahamu wengi waliobadilisha majina yao na kubadilika kabisa kutoka mfumo wa maisha walikua wanaishi nawe unaweza kubadilisha jina lako au kuzuia nguvu zile zinazoambatana na jina lako zisiambatane na maisha yako Mithali 22:1..” Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu”. 
Nguvu ya majina mabaya tuliyopewa na wazazi wetu zisifanye kazi kwenye maisha yetu!
Zaburi 58:3..”Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo”.
Isaya 48:8..”Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nalijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako”
Kwa wenye majina ya kizungu kama mimi basi cheki HAPA mfano CALVIN ni kutokana na jina la kifaransa Chauvin likimaanisha Kipara :-)
Kwa ujumla,Tukatae misingi mibaya ya majina yetu, tusimamishe kazi mbaya na kujenga majina yenye baraka na kibali katika maisha yetu. Barikiweni sana!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...