Sunday, June 17, 2012

Usiionee haya Injili ya Kristo, iende mbele


Huu ni wakati wa tofauti kabisa, huu sio ule wakati wa kumsubiria mtu mmoja tu ahubiri , wengine wakikaa na kumpigia makofi tu, Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto. Matendo 2:17 Huu ni wakati wa JESHI LA BWANA, watu hodari, wenye maarifa, Imara na watendaji zaidi si wa maneno matupu tu maana imeandikwa Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu 1Wakorintho 4:20…Roho tuliyepewa si wa kujivunia wala kutambia watu bali ni wa kazi na tunakuwa washindi sababu ya Roho mtakatifu “‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. Zekaria 4:6 huu ni wakati wa kila mtu awe mwana injili, kila mtu ASIIONEE HAYA injili, ni wakati wa kila mtu kuhubiri/kushare/kushuhudia/ kueleza/ kupasha habari…habari gani ? HABARI NJEMA! …

Ni kila mtu kutumia kila alicho nacho, kwa kila namna , na kila mbinu, kusema/kutenda/kuishi maisha yanayovuta wengine kwa Yesu… kwa kushirikiana, kwa kuhimizana….kwa sms, kwa Facebook, kwa mitandao, ana kwa ana, kwa Tshirts za maandishi, kwa ringtone, kwa sticker ya kwenye gari, kwa maandishi kwenye kikombe cha chai….Are you a winner? True Winner ni winner of souls….Kupunguza idadi ya watu wanaokwenda Jehanamu na iwe ni KIPAUMBELE cha kila mmoja…Kama kweli tunampenda Yesu basi tufanye kile ambacho Moyo wake wote upo hapo – “KUOKOA” roho…!!!!!++++!!!!!. Kama kweli unampenda Yesu utatafuta Pesa ya kupeleka Injili mbele, Utatumia uwezo na akili na ujuzi ulio nao kumwinua Yesu na kutetea Injili…Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia Warumi 1:16 – msemo huu uwe msemo wa kila mmoja!

–Pastor Abel, “B”family ministry!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...