Ijumaa Kuu, Pasaka!
Baada ya alhamis kupita, Ijumaa Bwana Yesu alipigwa mijeredi, alichubuliwa, alidharauliwa na kuteswa sana. Wakamcoma mkuki ubavuni, akafa na Jumapili siku ya tatu. Akafufuka. Yu hai hata leo, tunaishi naye!! Kwa kupigwa kwa Yesu sisi tumewekwa huru, tumehesabiwa haki bure pasipo sheria, magonjwa yetu, huzuni zetu alizibeba msalabani. Tumepona
Je kuna haja ya wakristo kukumbuka kuteswa na kifo cha Bwana Yesu Ijumaa Kuu? Kuna wakristo wengine hawali nyama, wengine wanahuzunika sana. Nk
Warumi 14:5 imeandika ” Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa ni sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe”
Tunaweza kuweka akilini mwetu kwamba siku hii ni siku ya kukumbuka kifo cha Bwana Yesu, Mateso aliyoyapata ni kwa ajili yetu, Damu yake ilimwagika msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.
1 Wakorinto 11:24-26 “Naye akisha kushukuru akaumega, akasema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo”
1 Petro 3:18 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa”
Wakristo wengi tunaikumbuka siku hii na pengine kuimba nyimbo za kuhuzunisha za kusulubiwa kwa Bwana Yesu, kufanya maombezi na kumshukuru Mungu.
Tunakumbuka siku ya kusulubiwa na kufufuka kwa Bwana Yesu maana Imani yetu iko hapo.
Ijumaa kuu zijazo:
2012 = April 6
2013 = March 29
2014 = April 18
2015 = April 3
No comments:
Post a Comment