Sunday, March 4, 2012

Ulimi Mzuri (Mithali 15:4).



Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo (Mithali 15:4).

Mithali 4:20-22 inatuonyesha umuhimu wa kulipa Neno la Mungu umakini mkubwa katika maisha yetu; inasema: “Mwanangu, sikiliza maneno yangu…Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.” “Safi,” kama ilivyotumika katika mstari wetu wa ufunguzi imetafsiriwa kutoka katika neno la Kiebrania “marpe,” ambalo maana yake ni uponyaji. Ni neno hilo hilo lenye tafsiri ya “afya” katika Mithali 4:22. Kwa hiyo, ulimi safi au “ulimi ulio “marpe” ni ulimi uponyao; ulimi unenao afya, uponyaji na uzima!
Sasa, ulimi unaweza kuwa wa uponyaji au wenye dawa pale unapokuwa umejazwa na Neno la Mungu!
Kumbuka, tumesoma katika Mithali 4:22 kwamba Neno ni afya (dawa) katika nyama au mwili wa mwanadamu. Hivyo ulimi unenao Neno la Mungu; ulimi mzuri; hunena afya, rutuba, ustawi na uzima katika mwili. Vile vile utagundua kwamba andiko hilo hilo linasema “…ukorofi wa ulimi huvunja moyo.” Ukorofi maana yake ni uharibifu au udanganyifu; ina maanisha kutokuwa na msimamo na kuchanganya maneno. Huitwa “kupingana” katika ulimi, na husababisha uharibifu au kidonda katika roho.
Wengi bila kujua huchubua au huumiza roho zao kwa kuongea vibaya pale maneno yao yanapokuwa hayaendani na jinsi Injili isemavyo. Roho ya mtu inapokuwa imechubuliwa sana kupitia maungamo mabaya, muda mfupi tu ujao, utajidhihirisha katika mwili. Michubuko au magonjwa mengi yanayopitia katika miili yao yalianzia katika roho zao.
Hii ndiyo maana kama mtoto wa Mungu, unatakiwa kupalilia ulimi ulio mzuri; jifunze kunena Neno la Mungu kwa ujasiri. Moja ya huduma ya Roho Mtakatifu katika maisha yako ni kutakasa maneno yako ili uweze kuwa na “marpe” au ulimi mzuri; ulimi ulio wa uponyaji! Ruhusu huduma hii ijidhihirishe moja kwa moja katika maisha yako; nena Neno la Mungu, na litumie Neno ili kuamua afya yako, mstakabali, mafanikio na ulinzi.
Ukiri
Maisha yangu ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, na ninatembea katika haki, ushindi, mafanikio, afya, ustawi na ukuu. Neno la Mungu limezaa afya ndani yangu; mimi ni ushuhuda wa neema na utukufu wa Mungu kutokana na adhari ya Neno katika maisha yangu. Haleluya!
somo zaidi:Mithali 18:21; Yakobo 3:2
KUJISOMEA MAANDIKO KILA SIKU
Mpango wa kusoma Biblia kwa mwaka 1 : Yoshua 10-12;Luka Mtakatifu 9:1-17
Mpango wa kusoma Biblia kwa miaka 2 : Warumi 2:16-29; Zaburi 65-67

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...